RC KUNENGE ATOA ONYO KWA WALIOPANGA KUFANYA VURUGU DAR, ASEMA WATAKAOVURUGA AMANI WATAKIONA CHA MOTO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, October 31, 2020

RC KUNENGE ATOA ONYO KWA WALIOPANGA KUFANYA VURUGU DAR, ASEMA WATAKAOVURUGA AMANI WATAKIONA CHA MOTO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. ABOUBAKAR KUNENGE ametoa onyo kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya vurugu ambapo ameeleza kuwa yoyote atakaejaribu kuvuruga amani kwenye mkoa huo atawajibishwa kwa mujibu wa Sheria.

RC KUNENGE ametoa onyo hilo wakati uzinduzi wa baraza la wafanyakazi wa shirika la uwakala wa Meli Tanzania TASAC ambapo amesema hali ya amani na utulivu kwenye jiji hilo ipo shwari na itaendelea kuwa shwari kwakuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri.



Wakati huohuo RC KUNENGE ametembelea ujenzi wa stand mpya ya kisasa ya Mbezi Louis na kukuta ujenzi huo ukiwa katika hatua ya upauaji ambapo amemuelekeza mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya November 30 kama Rais DKT. JOHN MAGUFULI alivyoelekeza.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages