TANZIA: MSANII WA BONGOFLEVA ALMAARUFU C PWAA AFARIKI DUNIA LEO JIJINI DAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, January 17, 2021

TANZIA: MSANII WA BONGOFLEVA ALMAARUFU C PWAA AFARIKI DUNIA LEO JIJINI DAR

 

Punde chumba chetu cha habari kimezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Msanii mkongwe wa Bongo Fleva Ilunga Khalifa almaarufu 'C Pwaa' ambaye amefariki alfajiri ya kuamkia leo akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa rasmi kutoka kwa ndugu wa karibu wa C Pwaa zinathibitisha CP kuugua ugonjwa wa Nimonia na alifikishwa hospitalini hapo kwa matibabu, hali yake haikuwa njema hadi umauti unamkuta alfajiri ya leo.

Aidha taarifa kutoka kwa mtu wake wa karibu zinaeleza kuwa msiba upo Magomeni Mikumi na kwamba maziko yake yatafanyika saa kumi.

Uongozi wa WOR'OUT MEDIA unaungana na Ndugu, jamaa na marafiki na Watanzania wote kwa ujumla  kuomboleza kifo cha 'Lijendari' huyu katika anga ya muziki wa Kizazi kipya.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages