GAMBO AAHIDI KUFUATILIA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA BARABARA YA BARACUDA-SORENYI KATA YA BARAA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, February 27, 2021

GAMBO AAHIDI KUFUATILIA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA BARABARA YA BARACUDA-SORENYI KATA YA BARAA





MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo ameendelea na ziara yake mtaa kwa mtaa ya kusikiliza kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na Mamlaka husika, ameyasema hayo wakati akitembelea Kata ya Baraa.

Akiwa katika ziara hiyo Mbunge amewaahidi wananchi wa Kata hiyo kuwa atakuwa mstari wa mbele na kutumia nguvu kubwa kuhakikisha barabara ya Barakuda Soreni ambayo imekuwa kero sana kwa wakazi wa mtaa huo nakusababishia kukosa baadhi ya huduma za kijamiii inatengenezwa na mamlaka husika.

Gambo ameendelea kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Jimbo la Arusha pamoja na kueleza mambo makubwa ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais DR. John Pombe Joseph Magufuli tangu achaguliwe mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages