GAMBO AWAPONGEZA AUWSA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, February 17, 2021

GAMBO AWAPONGEZA AUWSA


Na Mwandishi Wetu | Arusha | Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Mashaka Gambo ameipongeza Idara ya Maji AUWSA kwa namna wanavyoshirikiana naye katika kutatua kero mbalimbali za Maji katika Jiji la Arusha.

Gambo amezungumza hayo leo katika kikao kazi cha Waziri wa Maji Jumaa Aweso na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji ameeleza kuwa Idara ya maji kwa sasa wameanzisha kitengo maalumu mahususi ambacho kimeweza kuwasaidia wananchi wengi na kutatua kero zao kwa wakati.

Sambasamba na hayo Mbunge huyo amemueleza Waziri Aweso juu ya wakandarasi wa mradi wa maji Jijini hapa kwa kushindwa kurejesha miundombinu kama awali mara baada ya kufanikiwa kupitisha miundo mbinu hiyo ya maji.

Pia Gambo amemtaka Waziri Aweso kutatua kero kubwa ya muda mrefu ya wananchi wanaoishi jirani na kiwanda cha A to Z kuweza kuwajengea miundombinu mikubwa inayokidhi mahitaji ya eneo hilo kutokana na muda mwingine maji taka kutiririka kwenye makazi ya wananchi wa jirani na kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages