KABATI ATAKA WANAWAKE UWT KUANZISHA MIRADI YA KILIMO CHA BIASHARA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, February 21, 2021

KABATI ATAKA WANAWAKE UWT KUANZISHA MIRADI YA KILIMO CHA BIASHARA


Na Khalfan Akida | IRINGA | Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia CCM, Dkt. Ritta Kabati, amewataka wanawake UWT mkoani Iringa kuhakikisha wanajiingiza katika miradi ya kilimo ili kujikwamua kiuchumi kutokana na uwepo wa rasilimali kubwa ya ardhi yenye rutuba mkoa wa Iringa.

"Kwa sasa lazima sisi kama Umoja wa Wanawake tujikite katika kilimo cha biashara, tulime mbogamboga, tulime hata matunda ambapo kama tutauza basi tutajiingizia kipato katika jumuiya yetu na familia kwa ujumla"


Akizungumza katika baraza la UWT wilayani Kilolo, Kabati amesema kutokana na sera nzuri ya serikali ya sasa hususani katika kilimo cha biashara ipo haja ya wanawake mkoa wa Iringa kujikita katika kilimo cha matunda na mbogamboga ambacho tayari serikali imeonesha nia ya kuwasaidia wakulima nchini.

Aidha, Dkt. Ritta Kabati ameahidi kusaidia mkakati wowote wa Wanawake katika kilimo kwa kuwasaidia pembejeo pamoja na kusaidia vitendea kazi na maarifa ya wataalam wa masuala ya Kilimo kutoka wizarani.

"mimi nilishaanza hivyo kama na nyie mtaanza sitashindwa kuwasaidia vifaa vya utendaji kama trekta mlimie pamoja na kuwaletea wataalam wa kilimo kutoka wizarani"


Kwa upande wake mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM mkoa wa Iringa, Bi. Nicolina Lulandala amewaomba wanawake wote wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Iringa kuungana pamoja katika kuhakikisha viongozi pamoja na wadau wote wanaunga mkono juhudi za utekelezaji wa Ilani ya CCM ya uchaguzi 2020-2025.

"Sasa hivi muda wa makundi umeisha huu ni muda wa kazi tu, kwa sababu viongozi tuliowataka wote tumeshawapata cha msingi ni kufanya kazi ili kuwapa moyo hata viongozi wanaotaka kuungana ili kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa ufanisi"


Hata hivyo, Bi.Lulandala amewataka UWT mkoa wa Iringa kuendeleza Umoja huo katika kuanzisha miradi inayoweza kuwa na tija kiuchumi kwa Jumuiya, Chama na hata kwa mtu mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages