MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA BALOZI KIJAZI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, February 20, 2021

MAJALIWA AONGOZA MAZISHI YA BALOZI KIJAZI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitupa udongo kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika Mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Francisca Kijazi, Mjane wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi , Balozi John Kijazi katika Ibada ya kumwombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Augustino lililopo Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mawaziri wakiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi katika mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Augustino, eneo la Manundu Korogwe, Februari 20, 2021. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimwakilisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mazishi hayo. Kutoka kushoto ni; Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Juma Aweso, Waziri wa Maji, Ummy Mwalimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayesugulikia Muungano na Mazingira, Profesa Joyce Ndalicako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia na kulia ni Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages