Tanzia: Seneta wa Garissa Yusuf Haji aaga dunia - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, February 15, 2021

Tanzia: Seneta wa Garissa Yusuf Haji aaga dunia

  • Mbunge huyo alikata roho katika Hospitali ya Aga Khan alimokuwa akipokea matibabu
  • Mwanasiasa huyo mkongwe anaripotiwa kuanguka nyumbani kwake Garissa mnamo Septemba 29, 2020, na kuumia nyonga yake
  • Alisafirishwa hadi Nairobi na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan ambapo madaktari walipendekeza afanyiwe upasuaji
  • Mbunge huyo anatazamiwa kuzikwa katika Makaburi ya Kiislamu Lang'ata, Februari 15 mchana
Seneta wa Garissa Yusuf Haji ameaga dunia akiwa na miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mbunge huyo alikata roho katika Hospitali ya Aga Khan alimokuwa akipokea matibabu. Kulingana na familia yake, waziri huyo wa zamani alipumua pumzi yake ya mwisho Jumatatu, Februari 5 asubuhi.


Haji, ambaye aliteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta kuongoza Jopo Kazi la Maridhiano (BBI). alisafirishwa nchini Uturuki kwa matibabu mwishoni mwa 2020 lakini baadaye alirejea nchini. Mbunge huyo anatazamiwa kuzikwa katika Makaburi ya Kiislamu Lang'ata, Februari 15 mchana.

Kiongozi huyo wa muda mrefu aliongoza Bonde la Ufa mwaka 1970 hadi 1998 na kisha kuteuliwa bungeni mwaka 2002. Haji ambaye ni baba yake Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Yusuf Haji alichaguliwa tena kama Mbunge wa Ijara mwaka 2007.


Mwanasiasa huyo mkongwe anaripotiwa kuanguka nyumbani kwake Garissa mnamo Septemba 29, 2020, na kuumia nyonga yake.

Alisafirishwa hadi Nairobi na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan ambapo madaktari walipendekeza afanyiwe upasuaji. Upasuaji huo ulichukuwa muda wa saa tano na kisha mwenyekiti huyo wa Kamati ya Seneti kuhusu Masuala ya Kigeni na Usalama alilazwa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages