
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Akiba Commercial Benki Juliana Swai (kulia), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya kutangaza kuwa Benki ya Akiba imepata mbia wa kimkakati yaani strategic Investor ambaye ni National Banki of Malawi Kupitia mbia huyu Benki ya Akiba sasa inaweza kuimarisha mtaji wake na kukidhii vigezo vya Benki Mkuu kuhusiana na swala zima la mtaji hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya Benki hiyo iliyopo mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Dora Saria.
Nduguwanahabarikutokavyombombalimbali
MabibinaMabwana
WafanyakaziwenzanguwaAkiba Commercial Bank
Itifakiikizingatiwa!
Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwaajili ya siku njema ya leo. Pia napenda kuwashukuru nyote kwa mwitikio wenu na kufika kwenu kujumuika nasi siku ya leo. Karibuni sana.
Ndugu Wanahabari!
Akiba Commercial bank ni Benki ya kibiashara ambayo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1997 imekuwa ikitoa huduma zake kwa wateja wengi wakiwa ni wajasiriamali wadogo, wakati na wajuu (yaani Micro, Small and Medium entrepreneurs. (MSMEs)
Benki imeweza kuwafikia zaidi ya Watanzania 200,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, na pamoja na Makao makuu Dodoma.
Watanzania hawa wameweza kufaidika na huduma za mikopo mbalimbali ya kijasiriamali pamoja na amana za aina zote kuanzia watoto wadogo, vijana na watu wazima. Aidha, huduma za benki kupitia simu za mikononi yaani Akiba Mobile zimeleta unafuu na urahisi zaidi katika kuwafikia wateja popote pale walipo.
Ndugu wanahabari
Baada ya utangulizi huo ningependa sasa kutoa taarifa rasmi kuhusiana na mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya Benki ya Akiba ambayo itapelekea kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya kifedha.
Benki ya Akiba imepata mbia wa kimkakati yaani strategic Investor ambaye ni National Banki of Malawi. Kupitia mbia huyu Benki ya Akiba sasa imeweza kuimarisha mtaji wake na kukidhi vizuri vigezo vya Benki kuu kuhusiana na swalaz ima la mtaji wa uendeshaji wa Benki ya Kibiashara baada ya mbia wake NBM kuweka kiasi cha shilingi za Kitanzania zipatazo billion 17.
Lengo kuu la mkakati huu ni kuimarisha mtaji wa Benki kama nilivyosema hivi punde. Lakini pia benki imekuwa ikiangalia mahitaji ya soko lake na kuona kuwa kuna haja ya kupata mwekezaji au mbia wa kimkakati kwaajili ya kuifanya benki iwe imara zaidi nakuweza kuboresha huduma zake na kuanzisha huduma nyingi zaidi ambazo zinahitajika kwenye soko la Kitanzania.
Ndugu Wanahabari!
Kupitia Ubia huu naomba niwaahidi wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla mabadiliko makubwa na chanya katika huduma zetu na mifumo yetu ya utoaji huduma.
Tunaamini kuwa tutaweza kuwahudumia wateja wetu kwa weledi zaidi kupitia utalaamu na uzoefu wa taasisi mbili hizi bobezi kwenye sekta ya fedha. Pia, tunatambua mahusiano mazuri na undugu kati ya nchi hizi mbili na ambazo pia zina mahusiano makubwa ya kibiashara.
Faida mojawapo ya wazi ni kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kufanyabiashara kati ya nchi hizi mbili kupitia huduma za kifedha ambazo zitapatikana kwa urahisi zaidi. Aidha uwekezaji huu utausaidia pia kuwepo kwa mazingira wezeshi ya ufanyajibiashara kwa nchi ambazo zipo kusini mwa bara la Afrika wakiwepo wanachama wa SADC
Ndugu Wanahabari!
Malawi ni moja ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika zinazotumia bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la kibiashara.
NBM ambayo ilianzishwa mwaka 1971 baada ya muungano wa Barclays Bank DCO na Benki ya Standard ya Afrika Kusini, ni moja ya benki kubwa nchini Malawi inayotoa huduma za benki ikiwemo rejareja yaani Personal and Retail banking, wateja wakubwa, huduma za kibenki za uwekezaji na udalali katika soko la hisa na mitaji.
Naomba nihitimishe kwakusema kuwa sasa Akiba Commercial Benki imekuwa mhimili imara katika sekta ya fedha na imefungua ukurasa mpya kibiashara.
Nawakaribisha Watanzania wote wafike Akiba Commercial Bank ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali kwa maendeleo ya maisha yao na biashara zao.
Akiba Commercial Bank, benki kwa Maendeleo yako
Asantenikunisikiliza
No comments:
Post a Comment