RAIS MSTAAFU AIMWAGIA SIFA BENKI YA NBC - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, May 11, 2021

RAIS MSTAAFU AIMWAGIA SIFA BENKI YA NBC

Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Nd Theobald Sabi. Hafla hiyo ilifanyika katika bustani za Serena Hotel jijini Dar es Salaam pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Nd Aboubakak Kunenge pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa huo Alhaj Mussa Salum, Wateja wa NBC na wadau wengine.
Rais Mstaafu Jakaya mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Nd Theobald Sabi wakati akichukua chakula wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki ya hiyo. Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa Salum, pamoja na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Nd Aboubakak Kunenge.
Mkurungezi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wateja wa Benki ya NBC pamoja na wadau mabli mbali waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi wa wafanyakazi wa benki hiyo.

Rais Mtaafu wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Benki ya NBC awataka wananchi wa Dar es Salaam, kusherekea Sikukuu ya Eid il Fitr kwa amani bila kuharibu funga zao. Hafla hiyo ya kufuturisha ilifanyika katika bustani za Serena Hotel jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Aboubakar Kunenge, Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa Salum, wateja wa Benki ya NBC na wadau wengine.

Akizungumza wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Banki ya Taifa ya Biashara, NBC usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam, Rais Mstaafu Kikwete pia aliipongeza Benki ya NBC kuwa na bidhaa maalum kwa makundi mbali mbali bila kubagua imani za kidini hivyo kuongeza mshikamano ndani ya jamii.

Pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa huduma hizo nzuri, Rais Mstaafu Kikwete alisema kwamba Benki ya NBC iko mstari wa mbele katika kujenga uchumi jumuishi kutokana na bidhaa ambazo zinalenga watu wenye uwezo tofauti wa kifedha kuanzia yule wa juu mpaka wa hali ya chini kabisa.

Aidha amewapongeza Bank ya Taifa ya Biashara, NBC kwa kuweza kufuturisha waliofunga na kwamba wanapata thawabu sawasawa na waliofunga. "Niwapongeze kwa kuweza kufuturisha na Mwenyezi Mungu awabariki kwa mlichokifanya ni kitu kikubwa sana, kuna wengi hawajafikiria kuweza kuwafuturi lakini ninyi mmeweza bila kuangalia.” amesema Kikwete.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Taifa ya Biashara NBC. Nd Theobald Sabi, aliwashukuru wateja na wageni waliofika kwenye Iftari hiyo na kusema kwamba ni mmoja ya matukio muhimu katika kalenda ya benki hiyo na ni sehemu ya kuongeza uhusiano na ushirikiano na wateja wao.

Kwa muda mrefu benki yetu ya NBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa futari kwa wateja wake Tanzania bara na visiwani Zanzibar wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.” alisema Sabi.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Nd Theobald Sabi aliongeza kuwa benki hiyo ina huduma za kibenki zinazofuata taratibu za Sharia. “Huduma zetu za Islamic Banking zilianziswha. tangu mwaka 2010 na ni huduma za mbadala kwa wateja wetu wanaopenda kufanya miamala kwa kuzingatia sheria za Kiislamu. Huduma hizi zinawalenga wateja wakubwa, wadogo na wateja binafsi na zinapoatikaa katika matawi yote ya benki hiyo nchini.

Baadhi ya huduma alizogusia ni mikopo isiokuwa na riba na inayofuata sheria kwa wafanyabiashara na waajiriwa, huduma za amana za muda maalum zenye gawio la faida halali na Akaunti ya Akiba ya La Riba iliyounganishwa na mfuko wa bima wa Takahul inayochangia hadi 1m ya rambirambi kwa wanafamilia inpotokea mteja amefariki.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages