
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe Florence George Samizi anaendelea kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa dira ya maendeleo Jimboni kwake ambapo Ijumaa Julai 30, 2021 amehudhuria Baraza la madiwani la Halmashauri ya Kibondo ambapo pamoja na mambo mengine amepata nafasi ya kushuhudia utoaji wa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye matokeo ya darasa la 4 na Halmashauri ya Kibondo.

Dkt. Samizi anaendelea na ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa Muhambwe kwa imani yao kubwa kwake, kuwaeleza mipango mikubwa ya Bajeti ya Serikali kwa Jimbo la Muhambwe na kuendelea kujitoa kwenye kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo Jimboni kwake.

No comments:
Post a Comment