BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA QATAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, August 5, 2021

BALOZI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA QATAR

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam | WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadili masuala ya kuimraisha uhusiano wa kidiplomasia, kuendeleza biashara na uwekezaji katika sekta za sekta za Madini, Utalii, pamoja na Mafuta na Gesi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid yakiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Balozi wa Qatar nchini Mhe. Hussain Ahmad Al Homaid wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara pamoja na Ubalozi wa Qatar.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages