BENKI YA NMB YASHINDA TUZO MBILI ZA UMAHIRI KIMATAIFA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, August 3, 2021

BENKI YA NMB YASHINDA TUZO MBILI ZA UMAHIRI KIMATAIFA


BENKI ya NMB imeshinda tuzo mbili za Kimataifa za umahiri kwa kutambulika kuwa benki bora nchini, ushindi uliotolewa na majarida makubwa duniani yanayoaminika katika kufanya tafiti za kifedha na mabenki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema, tuzo ya kwanza iliyotolewa kwa benki hiyo ni tuzo ya EuroMoney ambayo ni mara ya tisa kwa benki hiyo kushinda tuzo hiyo kutokana na ufanisi, utendaji na ubunifu wa benki hiyo.


Amesema, tuzo ya pili iliyotolewa na jarida la Global Banking and Finance imeitambua benki ya NMB kwa huduma bora kwa wateja binafsi na biashara za kati kwa mwaka 2021.

Zaipuna amesema kuwa hiyo ni heshima kubwa na kielelezo cha ufanisi wa benki hiyo na wameheshimu na kuthamini heshima hiyo na tuzo hizo zinatokana na juhudi zinazofanywa na benki hiyo na kutambuliwa ndani na nje ya nchi.

Kuhusiana na vigezo vilivyotumika na benki hiyo kuibuka kinara, Zaipuna amesema vigezo hivyo ni pamoja na ufanisi na utendaji, usalama wa huduma za kimtandao, mtaji na uwajibikaji wa benki hiyo kwa jamii.

Pia amesema benki hiyo itaendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuhakikisha wanatoa huduma bora na viwango vya juu kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages