DC.BASILLA AAGIZA KUKAMATWA NA KUWEKWA NDANI KWA WAKUU WA IDARA MBILI WILAYANI KOROGWE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, August 27, 2021

DC.BASILLA AAGIZA KUKAMATWA NA KUWEKWA NDANI KWA WAKUU WA IDARA MBILI WILAYANI KOROGWE


Na: MAWANDISHI WETU, KOROGWE | MKUU wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi, ameagiza kukamatwa na kuwekwa ndani kwa wakuu wa idara mbili ambao ni idara ya mipango na takwimu akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya manunuzi Yasin Msangi na mkuu wa idara ya manunuzi ambaye ni katibu wa kamati ya manunuzi Gregory Matandiko, kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za serikali kukiuka taratibu za manunuzi katika miradi hiyo.

Uwamuzi huo umetokana na ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Basilla Mwanukuzi aliyoifanya siku Jumatano Agost 25, akiambatana na kamati ya usalama ya wilaya katika miradi ya ujenzi wa jengo la utawala na Hospitali ya wilaya Makuyuni.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Mhe Basilla amesema katika dhiara hiyo hakuridhishwa na ujenzi wa wodi tatu unafanyika katika eneo hilo, na usimamizi wa miradi mingine hivyo baada ya kukaa kikao cha ndani na kamati ya usalama wilaya, kamati zote za

ujenzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Korogwe, wakafikia uwamuzi wa kuwa kamata wakuu wa idara hizo.

"Kaika dhiara niliyofanya nimegundua changamoto zinazosababisha kukwamisha miradi kutokamilika ni baadhi ya watendaji ,nimeagiza kukamatwa kwa wakuu wa idara husika pia nimemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya kuvunja kamati zote na kuteua wajumbe wapya katika idara hizo," anasema Mhe. Basilla.

Katika hatua nyingine Mhe. Mkuu wa Wilaya ameagiza kusimama kwa shughuli zote za ujenzi wa miradi hiyo kwa kipindi cha siku 14 ili kujiridhisha na matumizi ya fedha zilizotumika hadi sasa katika miradi hiyo.oo

Aidha Mhe. Basilla Mwanukuzi amemuagiza Kamanda wa Takukuru, kuanza kufanya uchunguzi wa swala hilo kunusuru fedha za serikali zinazoibwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages