Mgombea Wa Upinzani Ashinda Uchaguzi Wa Urais Zambia - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, August 16, 2021

Mgombea Wa Upinzani Ashinda Uchaguzi Wa Urais Zambia


Baada ya kupoteza uchaguzi mara tano, kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ameibuka mshindi wa uchaguzi mkuu .

Alikuwa akikabiliana na mpinzani wake wa siku nyingi Edgar Lunguambaye alidai kwamba uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki baada ya kupoteza kura nyingi katika ngome zake .

lilikuwa jaribio la sita la bwana Hichilema katika kuwania urais.

Wafuasi wake wamekuwa wakisherehekea katika barabara za mji mkuu wa Lusaka.

Bwana Lungu alisema kwamba maafisa wa chama chake cha Patriotic Front walifukuzwa kutoka katika vituo vya kupigia kura , wakiwacha kura bila ulinzi wowote.

Lakini kikijibu madai hayo chama cha bwana Hichilema cha United Party for National Development kilisema kwamba taarifa hiyo ni hatua za mwisho za utawala unaondoka.

Baada ya kujumlisha kura zote tume ya uchaguzi ilisema kwamba bwana Hichilema alishinda kwa kujipatia kura 2,810,777 huku Lungu akijipatia 1, 814, 201 katika uchaguzi huo wa siku ya Alhamisi.

Kulikuwa na jumla ya wapiga kura milioni saba waliojisajili kushiriki katika uchaguzi huo.

Ushindi huo mkubwa unaamanisha kwamba bwana Hichilema hatoshiriki katika awamu ya pili ya uchaguzi.

"Natangaza kwamba Hichilema ndiye rais wa Zambia", alisema mwenyekikti wa tume hiyo Esau Chulukatika kituo cha kutoa matokeo kilichopo mjini Lusaka.

Uongozi wa miaka sita wa bwana Lungu ulikosolewa kwa madai ya kukiuka haki za binadamu, ufisadi na uchumi uliodorora pamoja na ukosefu wa ajira.

Waandishi wa habari wanasema kwamba bwana Hichilema mwenye umri wa miaka 59, alipata kura za wapiga kura wengi ambao hawakufurahia uongozi wa Lungu.

Kwa sasa anakabiliwa na changamoto ya kuubadilisha uchumi wa taifa hilo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages