OFISI YA BUNGE YAKANUSHA WABUNGE KUTOKULIPA KODI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, August 3, 2021

OFISI YA BUNGE YAKANUSHA WABUNGE KUTOKULIPA KODI


OFISI ya Bunge yatoa ufafanuzi juu ya taarifa za upotoshaji zilizoenea katika mitandao ya kijamii katika siku za hivi karibuni zinazodai kwamba Waheshimiwa Wabunge hawalipi kodi kwenye mishahara yao.

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge leo Agosti, 3, 2021 jijini Dodoma inajulisha umma kwamba Waheshimiwa Wabunge kama ilivyo kwa Watumishi wengine wa umma na Viongozi wa Kisiasa wanakatwa kodi zote stahiki kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kodi ya mapato (PAYE) inayokatwa kwenye mishahara ya Wabunge.

Hivyo taarifa hiyo imeeleza kuwa umma upuuze taarifa hizo na tunatoa wito kwa Vyombo vya Habari hususan mitandao ya kijamii kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya Uandishi wa Habari ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Mamlaka husika ili kupata ukweli kabla ya kutoa taarifa kama hizi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages