RC Shinyanga azuia tani 400 za dengu kusafirishwa - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, August 25, 2021

RC Shinyanga azuia tani 400 za dengu kusafirishwa

Na Peter Saramba, Mwanza | Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk Phillemon Sengati amezuia zaidi ya tani 400 za dengu zinazodaiwa kununuliwa kutoka kwa wakulima kwa njia ya ulanguzi zisisafirishwe nje ya mkoa huo.

Dk Sengati ameagiza shehena hiyo ambayo ilikuwa imepakiwa kwenye malori tayari kwa kusafirishwa, ishushwe na kuhifadhiwa kwenye magala ya Vyama vya Msingi vya Ushirika (Amcos) na Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (Shirecu) kusubiri mnada.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii wa gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu leo Agosti 24, Dk Sengati amesema uamuzi huo siyo tu unalinda maslahi ya wakulima watakaopata bei nzuri na yenye ushindani, bali utawezesha halmashauri na Amcos kupata mamilioni ya fedha kupitia ushuru.

"Hatujataifisha mazao hayo kama baadhi ya watu wanavyoeneza na kupotosha kupitia njia ya mitandao ya kijamii; Serikali ya mkoa imeagiza mazao yote yahifadhiwe kwenye maghala ya ushirika na yauzwe kwa njia ya mnada kama ilivyo maelekezo ya Serikali ya mwaka 2019 yaliyosisitizwa tena mwaka 2020," amesema Dk Sengati

Ameongeza; "Mimi sina maelekezo au mwongozo mwingine kuhusu ununuzi wa mazao ya dengu, ufuta, choroko na mbaazi zaidi ya njia ya mnada kupitia Amcos. Hilo ndilo nalisimamia,"

Amesema mazao yote yanayohifadhiwa katika maghala ya Amcos na Shirecu yataanza kuuzwa kesho Jumatano Agosti 25 kwa njia ya mnada kupitia Soko la mnada kwa njia ya mtandao.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages