UJENZI WA VITUO VYA AFYA 150 NA UKAMILISHAJI WA VYUMBA VYA MADARASA 560 KUTOKA KATIKA TOZO YA MAWASILIANO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, August 20, 2021

UJENZI WA VITUO VYA AFYA 150 NA UKAMILISHAJI WA VYUMBA VYA MADARASA 560 KUTOKA KATIKA TOZO YA MAWASILIANO


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imepokea fedha kutoka katika tozo ya Mawasiliano kiasi cha Shilingi Bilioni 22.5 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 90 katika Tarafa ambazo hazina vituo vya Afya na tarehe 23 Agosti, 2021 itapokea kiasi cha Shilingi biilion 15 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya Afya 60 na hivyo kufanya jumla ya Vituo vya Afya vitakavyojengwa kutokana na tozo ya mawaliano kuwa 150.

Halkadhalika OR-TAMISEMI tarehe 23 Agosti, 2021 itapokea tena kiasi cha Shilingi bilioni 7 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarsa 560 katika shule za Msingi na Sekondari nchini.

Kufuatia upatikanaji wa fedha hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuwa:-

1. Ujenzi wa Vituo vya Afya na ukamilishaji wa vyumba vya madarsa uanze mara moja ndani ya wiki mbili mpaka mwezi mmoja baada ya kupokea fedha za ujenzi na utekelezaji wa ujenzi usizidi miezi mitatu;

2. Majengo yanayopaswa kuanza kujengwa kwa upande wa Afya ni Jengo la Wagonjwa wa Nje, Maabara na Kichomea Taka;

3. Ujenzi wa miradi hii utumie Force account na sio Mkandarasi “Fedha hizi ni vyema zikarudi kwenye Jamii husika; na

4. Vituo vya Afya vijengwe kwenye Makao Makuu ya Tarafa ambayo haina Kituo cha Afya na kama Tarafa hiyo ina Hospitali ya Halmashauri basi Halmashauri ichague Kata ya kimkakati ndani ya Tarafa hiyo kujenga Kituo cha Afya

Nteghenjwa Hosseah

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Ofisi ya Rais – TAMISEMI

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages