RC MAKALLA ALITANGAZA ENEO VOLCANO YA TOPE KUNDUCHI NI HATARISHI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, October 12, 2021

RC MAKALLA ALITANGAZA ENEO VOLCANO YA TOPE KUNDUCHI NI HATARISHI

  • Asema eneo hilo halifai kwa makazi.
  • Awataka Wananchi wa eneo husika kuchukuwa tahadhari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelitangaza eneo la Kunduchi lenye Volcano ya Tope kuwa eneo la hatari na halifai kwa makazi na kuwataka Wananchi wa familia Tisa ambazo makazi yao yameathiriwa kuanza kuchukuwa tahadhari.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea na kukagua eneo hilo kujionea athari za Volcano hiyo na kulielekeza Jeshi la Polisi kuweka uangalizi Katika eneo hilo.

Aidha RC Makalla amesema taarifa ya kitaalamu iliyowasilishwa ofisini kwake inaeleza kuwa eneo hilo halifai kwa makazi ndio maana amefika kuwataka kuchukuwa tahadhari wakati Serikali inaangalia hatua za kuchukuwa.


Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza eneo hilo kuwekewa alama za tahadhari ili kuwaepusha wananchi na maafa.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages