SIMBA YAIVURUGA GALAXY - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Sunday, October 17, 2021

SIMBA YAIVURUGA GALAXY


Mwandishi wetu | MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba leo wameibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza uliopigwa Botswana.

Simba ilianza kupata bao la kwanza dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa kiungo wake Taddeo Lwanga aliyepiga shuti kali baada ya mpira wa kona uliopigwa na Rally Bwalya na kimalizia na John Bocco .

Katika dakika ya 6 simba ilifanikiwa kuongoza bao la pili lililofungwa na nahodha wa timu hiyo John Bocco.
Baada ya mabao hayo mawili ya mapema, Galaxy walianza kutafuta mabao ya kusawazisha lakini walijikuta wakikwama kwenye ukuta wa Simba uliokuwa unalindwa mabeki'.

Matokeo hayo yanakuwa na faida kubwa kwa Simba kwani Jwaneng watakuwa na kibarua kizito cha kupindua matokeo wakati watakapokuja kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Octoba 24, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages