STARS YAPOTEZA NYUMBANI 1-0 DHIDI YA BENIN - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, October 7, 2021

STARS YAPOTEZA NYUMBANI 1-0 DHIDI YA BENIN


Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM | KIKOSI cha Stars leo imepokea kichapo kwa Benin katika mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe La Dunia 2022 nchini Quartar, katika mchezo uliopigwa dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika kipindi cha kwanza timu zote zilipambana lakini hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzie.

Katika dakika za 70 aliyefunga bao ni steven Mounie ambaye alipachika kwa shuti kali akiwa nje ya 18.

Huku jitihada za Stars kupata bao zilikwama ambapo mshambuliaji John Bocco alikosa nafasi ya wazi akiwa ndani ya 18 kwa kushindwa kufunga baada ya shuti lake kuokolewa na kipa wa Benin.

Ni mchezo wa kwanza Stars kupoteza katika kundi J na wanapoteza pointi tatu wakiwa katika Uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wake.

Kwenye msimamo sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na vinara ni Benin wenye pointi 7.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages