
- Wampongeza mkuu wa mkoa kwa ushawishi Na kuwashirikisha
- Uongozi machinga wafanikisha zoezi Usiku wa kuamkia leo
- Mitaa ya Msimbazi na Gerezani iyokuwa imejaa Vibanda Sasa Barabara za watembea kwa miguu zinapitika
- Wananchi wapongeza zoezi Hilo
- Machinga wataka maeneo waliyoondoka yalindwe yasivamiwe upya
Siku moja baada ya kumalizika kwa muda wa siku 12 zilizoongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla kwa Wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara maeneo yaliyokatazwa kuhama, Zoezi la kuondoa Vibanda maeneo ya Msimbazi na Gerezani limefanyika kwa ushirikiano wa Wafanyabiashara hao usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Msemaji wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam Masoud Isa amesema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa Kutokana na elimu iliyotolewa na Serikali na Viongozi wa Machinga.
Aidha Msemaji huyo ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha maeneo yote walipoondoka Machinga yanalindwa ili yasivamiwe upya.
Nao baadhi ya Wananchi waliofika Soko la Kariakoo kufanya Manunuzi akiwemo Ashura Ally amepongeza Serikali kwa kutatua kero ya Biashara holela Jambo lililokuwa likisumbua watembea kwa miguu.
No comments:
Post a Comment