WACHEZAJI GUINEA BISSAU WAUGUA MATUMBO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, October 6, 2021

WACHEZAJI GUINEA BISSAU WAUGUA MATUMBO

KATIKA hali ya kushangaza! Wachezaji wa timu ya taifa ya Guinea Bissau wamejikuta kuugua matumbo huku wakiharisha na kutapika baada ya kula chakula cha jioni hapo jana wakiwa kambini nchini Morocco kujiandaa na mchezo wao wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya timu hiyo.

Awali taarifa iliripotiwa kuwa idadi ya Wachezaji 25 wanaugua matumbo na baadae ilifahamika kuwa ni idadi ya Wachezaji Sita pekee waliokutwa na kadhia hiyo na tayari wapo Hispitali kwa matibabu zaidi.

Mchezo wao dhidi ya Morocco unatarajiwa kuchezwa leo majira ya Saa 4:00 Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki na Kati.

Timu hizo zipo Kundi moja, Kundi I na timu za Morocco, Guinea na Sudan. Huku Guinea Bissau wakiongoza Kundi wakiwa na alama nne, Morocco alama tatu, Guinea alama moja na Sudan hawana alama yoyote.



No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages