LEO NI KUMBUKIZI YA SIKU YA WACHAGA DUNIANI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, November 10, 2021

LEO NI KUMBUKIZI YA SIKU YA WACHAGA DUNIANI


Leo Ni Sikukuu ya Wachagga Duniani (World Chagga's Day),

Ni siku kubwa Iliyokuwa Inaadhimishwa kila Mwaka Siku Ya Novemba 10,

Miaka ya kabla ya Uhuru wa Tanganyika na miaka michache Baada ya Uhuru wa Tanganyika. Siku hii Ilisherehekewa Kitaifa Kilimanjaro katika Ikulu ya Mangi Mkuu wa Wachagga KDC Moshi Mjini na Katika Maeneo mengine ya Wamangi Kilimanjaro nzima.

Maadhimisho haya yaliyohudhuriwa na Watu wa Rika zote kuanzia Watoto, Wanafunzi wa Shule na Watu Mashuhuri kutoka ndani na Nje ya Kilimanjaro. Yalijumuisha maonyesho mbalimbali na Nyimbo ukiwemo Wimbo wa Jamii / Taifa La Wachagga Kilimanjaro.

Baadhi ya Wachagga wa leo wenye angalau kuanzia miaka 70 na kuendelea bado wana Kumbukumbu ya Maadhimisho haya ambayo Yalikuwa muhimu na makubwa sana Kilimanjaro.
Siku hii Ilikuwa maalum kwa ajili ya kuimarisha Mshikamano, Ushirikiano, Kujiamini na Kujitambua kwa Wachagga katika kukuza ustawi wa Wachagga Kuelekea Kutimiza Ndoto Kuu Ya Wachagga (Chagga Dream).

Sisi Wachagga wa leo, kama ilivyo kwa Jamii nyingi zenye kujitambua Duniani Tuna Haki na Wajibu wa Kuienzi siku hii muhimu kwetu itakayosaidia Kuimarisha Mshikamano, Ushirikiano, Kujiamini na Kujitambua kwa ajili ya Ustawi wa Jamii yetu ya Sasa na Vizazi vinavyokuja.

Hivyo wewe kama Mchagga Mzalendo.

Tuma Ujumbe huu kwa Mchagga yeyote, anaweza kuwa Mzazi, Ndugu, Rafiki, Jamaa au Jirani.
Ujumbe: "(HERI YA SIKUKUU YA WACHAGGA, Siku hii muhimu sana kwetu ikarudishe Mshikamano na Upendo Baina Yetu na Kutujengea Kujiamini na Kujitambua zaidi)"

Message: "(HAPPY CHAGGA'S DAY, May This Special Day of Ours Bring Back Our Cohesion and Love Among Us and May it Bring Confidence and Enlighten Us More)".

Kwa kutuma Ujumbe huu utakuwa umefanya Jambo Kubwa la Kizalendo Kwa Jamii yetu kwa kusambaza Upendo na Mshikamano.

Wewe pia unaweza kuisherehekea siku hii kwa Kupika Vyakula Vya Asili Ya Kilimanjaro, Kusikiliza Nyimbo Zetu za Asili na Kuzungumza na Watu Hasa Watoto Hadithi Mbalimbali Zilizotuletea Ufahari na Ushujaa Mwingi Kilimanjaro.

NAWATAKIENI WOTE HERI YA SIKUKUU YA WACHAGGA,

Siku Hii Ikawe Ya Tofauti Sana Kwenu na Ikaache Kumbukumbu Muhimu za Upendo na Mshikamano.

HAPPY CHAGGA'S DAY TO YOU ALL.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages