
Makampuni sita ya magari yameahidi kuacha kutengeneza magari yanayotumia mafuta ifikapo mwaka 2040, kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya Uingereza ambayo ndio mwenyeji wa mkutano wa Tabianchi wa COP26.
Lakini duru zinazohusika na makubaliano hayo zimesema makampuni mawili makubwa ya magari ya Toyota na Volkswagen hayakusaini makubaliano hayo.
Aidha kampuni ya Sweden ya Volvo imesema inajiandaa kutengeneza magari yanayotumia umeme tu ifikapo mwaka 2030.
Uingereza, imesema nchi nyingine nne zikiwemo New Zealand na Poland zimejiunga na mataifa ambayo tayari yamejitolea kuhakikisha magari yote mpya yatakuwa hayatoi gesi chafu hewani ifikapo mwaka 2040.
No comments:
Post a Comment