RC MAKALLA AIPA MAMBO MATANO TMDA KUDHIBITI WIZI WA DAWA NA DAWA BANDIA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, November 30, 2021

RC MAKALLA AIPA MAMBO MATANO TMDA KUDHIBITI WIZI WA DAWA NA DAWA BANDIA

 
  • Awataka Kudhibiti Wizi wa Dawa za Serikali na kutokomeza Dawa Bandia.
  • Asisitiza kufanyika kwa ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kudhibiti wezi wa dawa Na dawa bandia.
  •  Ataka "vishoka" ambao ni wakaguzi feki kukomeshwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA kupatia ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali na kutoa onyo kwa Maduka yanayonunua dawa za Wizi.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Mafunzo ya siku tano kwa Wakaguzi wa Dawa wa Manispaa za Mkoa huo yaliyolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa.
Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeji wa kazi hiyo ambayo inabeba dhamana ya Maisha na uhai wa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka Wanaofanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa ili kubaini wababaishaji na kutaka uwepo wa watoa huduma Wenye sifa na Vigezo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages