RC MAKALLA AMPONGEZA HAJI MANARA KWA KUUNGA MKONO KAMPENI YA USAFI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, November 26, 2021

RC MAKALLA AMPONGEZA HAJI MANARA KWA KUUNGA MKONO KAMPENI YA USAFI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amempongeza Msemaji wa Yanga Haji Manara kwa tamko lake la kuunga mkono kampeni ya usafi mkoa Dar es salaam.

RC Makalla ameyasema hayo leo wakati wa kikao Cha watendaji wa Mitaa Na Kata kilichofanyika ukumbi wa Diamond jubilee kujadili mikakati ya kufanikisha usafi endelevu Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa amempongeza Haji Manara Na wanayanga wa matawi yote kwa namna walivyopanga kuhamasishana kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.


Aidha RC Makalla amesema Jambo la usafi ni jukumu la kila mtu na kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi Disemba 04 ili kushirikiana kufanya usafi wa pamoja.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages