RC MAKALLA AWAOMBA WANANCHI DSM KUHUDHURIA KWA WINGI SHEREHE ZA UHURU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, November 26, 2021

RC MAKALLA AWAOMBA WANANCHI DSM KUHUDHURIA KWA WINGI SHEREHE ZA UHURU

 

- Afanya kikao Na Watendaji wa Mitaa Na Kata kuomba kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi.


- Maadhimisho ya kwanza  ya sherehe za Uhuru kwa awamu ya sita.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zinazotaraji kufanyika Disemba 09 kwenye Uwanja wa Uhuru.


RC Makalla ametoa wito huo wakati wa kikao Cha pamoja na Watendaji wa Kata na Mitaa kilichoketi leo kuweka mikakati ya Maandalizi ya Sherehe hizo ambazo zitakuwa za kwanza kwa Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Aidha katikati kuelekea Sherehe hizo zitatanguluwa na uzinduzi wa Miradi mbalimbali ya maendeleo.



Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zitahudhuriwa na Wakuu wa Nchi mbalimbali watakaowasili nchini kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages