TADB Yatoa Mikopo Ya Zaidi Ya Shilingi Bilioni 391 Kwa Sekta Ya Kilimo - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, November 10, 2021

TADB Yatoa Mikopo Ya Zaidi Ya Shilingi Bilioni 391 Kwa Sekta Ya Kilimo

Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imefanikiwa kutoa mikopo yenye jumla ya thamani ya zaidi shilingi bilioni 391 kwa ajili ya kuendeleza Kilimo na imeaahidi kuendelea kutoa mikopo zaidi.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa TADB Frank Nyabundege alisema lengo la benki hiyo ni kuwafikia wakulima wengi zaidi

Mkurugenzi huyo alisema ili kuwafikia wakulima wengi zaidi,benki hiyo imekuwa ikichagiza mabenki ya biashara kukupesha wakulima kupitia dhamana ambazo benki hiyo imekuwa ikitoa kwa mabenki mbali ya biashara ya mtandao mpana nchi nzima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Frank Nyabundege(kushoto) akipata maelezo juu ya shughuli za kiwanda cha kuzalisha maziwa cha Tanga Fresh kutoka kwa maofisa wa kiwanda hicho ambao walishiriki katika maonyesha ya wiki ya huduma za kifedha jijini Dar es Salaam. Kiwanda cha Tanga Fresh ni moja kati ya wanufaika wa mikopo inayotolewa na benki ya kilimo.
Meneja wa Mfuko wa Dhamana kwa wateja wadogo wa Benki ya Kilimo (TADB), Asha Tarimo (kushoto), akimuelekeza faida ya kutumia benki hiyo mteja aliyetembelea banda la benki hiyo, Yahaya Duru, katika maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.
Wateja waliotembelea banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakipata maelezo ya shughuli mbali mbali ambazo zinafanywa na baadhi ya wanufaika wa mikopo inayotolewa na benki hiyo katika maonyesho ya huduma za kifedha yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages