TRA PWANI YAFUNGA KIWANDA BUBU CHA MABOMBA YA MAJI KIBAHA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, November 10, 2021

TRA PWANI YAFUNGA KIWANDA BUBU CHA MABOMBA YA MAJI KIBAHA

Na Khadija Kalili, Kibaha | Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Pwani (TRA) Godwin Barongo amekifunga kiwanda bubu Cha mambomba ya maji kilichogundulika kuwepo katika maeneo ya Miembesaba Kata ya Kongowe Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

"Jana jioni tulipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari kutakuwa na kikao maalumu na baada ya kufika ofisini kwake leo asubuhi akatueleza kuwa kuna kiwanda Cha kutengeneza mambomba ya maji ambacho hakina usajili wa aina yeyote katika eneo hilo."

Tumechukua jukumu la kuja katika kiwanda hiki ambacho hakuna Ofisi, Mneja ila wapo vijana wachache ambao wamekua wakiendelea na uzalishaji wa mabomba ambayo tumeelezwa kuwa mambomba hayo hupelekwa Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

"Leo hii tutahesabu mabomba na malighafi zote zilizomo ndani ya kiwanda hiki na baada ya hapo tutamwita muhusika Ili aje atuthibitishie kama yeye ni mlipa kodi halali aje na vithibitisho vyote kama amesajiliwa licha ya kupekua hatujapata nyaraka za aina yeyote ambazo zingetusaidia kumtambua muhusika" alisema Barongo.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Pwani RPC Nyigesa Wankyo alisema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema pia Mara baada ya kukagua ndani ya kiwanda hicho walikuta kiitabu kilicho andikwa Tiger Investment Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi Ili kuweza kumpata mmiliki .

Inspekta kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) Venance Colman alisema amefika hapo pamoja na Kamati iliyoundwa na RC Kunenge kuwa bahati mbaya hawana nyaraka za aina zinzoonyesha jina la mzazlishaji lakini wanazalisha mambomba ya maji hivyo sisi tuta chukua sampuli za bidhaa zote na kwenda kuzipima na kuangalia kama bidhaa zote zinazozalishwa kitandani hapo zinakidhi viwango na kama hazikidhi matakwa ya viwango hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika.

Hata hivyo Mkurugenzi Jupiter Investment Vincent Meena amekanusha kuwa kiwanda hicho siyo bubu kwani wanavyo vibali vyote halali vya uendeshaji wa kiwanda na wako tayari kuviwasilisha kwa Jeshi la Polisi Pwani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages