JUMUIYA YA MABOHORA WAMKABIDHI RC MAKALLA VIFAA KWAAJILI YA KAMPENI YA USAFI DSM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, December 3, 2021

JUMUIYA YA MABOHORA WAMKABIDHI RC MAKALLA VIFAA KWAAJILI YA KAMPENI YA USAFI DSM

  • Asema Maandalizi yote ya kuelekea Disemba 04 kwenye Uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Dar es salaam yamekamika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amepokea Vifaa vya Usafi ikiwemo Vifaa vya kuhifadhi taka na Fagio kutoka kwa Jumuiya ya Mabohora Kama sehemu ya kuunga mkono Kampeni ya Kusafisha na Kupendezesha Dar es salaam.

Akipokea Vifaa hivyo RC Makalla amewashukuru Mabohora kwa kutekeleza ahadi waliyoitoa Wakati wa Uzinduzi wa Mkakati endelevu wa Usafi Uliofanyika November 22.
RC Makalla amesema katika kuelekea Uzinduzi wa Kampeni hiyo Jumamos ya Disemba 04, Maandalizi yote yamekamika na kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza kufanya Usafi wa pamoja kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora, Murtaza Adamjee amesema Jumuiya hiyo ipo bega kwa bega na RC Makalla kufanikisha Kampeni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages