- Kudhibiti ufanyaji Biashara holela, kutunza bustani, kusafisha Na kuondosha takataka kwa wakati.
- Asema Serikali Na wadau itaendelea kuweka Dustibins maeneo ya stendi, masoko, hospitalini Na wenye mabus wametakiwa kuwa Na dustbins.
- Ni marufuku kuiba Vyuma, Minyororo na kufanya Biashara kwenye bustani zilizozungushiwa Minyororo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amefanya kikao Cha pamoja na Watendaji wa Kata na Mitaa yote ya Mkoa huo na kuwapatia maelekezo 7 ya kufanyia kazi ili kufanikisha Kampeni ya Usafi endelevu Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa kikao kazi hicho kilichofanyika ukumbi wa Diamond jubilee, RC Makalla amewataka Watendaji hao Kudhibiti kero ya Garage bubu na Car wash zinazoibuka kila kukicha kwenye hifadhi ya Barabara.
Aidha RC Makalla amepiga marufuku Ufanyaji wa Biashara kwenye bustani na Vyuma vilivyowekwa pembezoni mwa Barabara huku akiwaonya Wenye tabia ya kuiba Vyuma hivyo.
Ili kuhakikisha kila Mtendaji kuanzia ngazi ya Mtaa hadi kata anasimamia kikamilifu suala la Usafi, RC Makalla ametoa fomu Maalumu ya kupima uwajibikaji Kama Usafi unafanyika kuanzia ngazi ya Mtaa hadi kata na Mkoa utakuwa ukipokea marejesho kupitia fomu hiyo na kufanya ufuatiliaji Kama kile kilichojazwa kwenye fomu kinaendana na uhalisia wa Usafi.
Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Watendaji hao kuhakikisha maeneo wanayosimamia yanakuwa Safi muda wote, Taka zinaondolewa kwa wakati, huku akiwataka Kudhibiti Biashara holela kwa kuzuia Wafanyabiashara wasirudi upya kwenye maeneo yaliyokatazwa.
Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TARURA, TANROAD na DAWASA kumpatia Mpango wa kuonyesha Ni kwa namna gani Taasisi zao zinashiriki katika Kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment