RC MAKALLA AZINDUA MATOKEO YA RIPOTI YA UTAFITI WA SEKTA ISIYO RASMI MKOA WA DSM - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, December 20, 2021

RC MAKALLA AZINDUA MATOKEO YA RIPOTI YA UTAFITI WA SEKTA ISIYO RASMI MKOA WA DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezindua Matokeo ya utafiti wa sekta isiyo rasmi wa mwaka 2019 Mkoa wa Dar es salaam ambapo ripoti hiyo imeshauri kurasimishwa kwa biashara zisizo rasmi ili kuchangia Pato la Taifa Baada ya kubaini Shughuli zisizo rasmi haziingizii Pato lolote serikalini.

Akizindua Matokeo ya utafiti huo, RC Makalla amesema Serikali inakwenda kufanyia kazi Mapendekezo yote yaliyotolewa na ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS kupitia utafiti huo ili Shughuli hizo ziweze kuleta tija.

Aidha RC Makalla amesema kupitia taarifa ya utafiti huo imewezesha Mkoa kujua changamoto na Fursa za kufanyia kazi ili kuongeza makusanyo ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Dar es salaam unachangia Asilimia 18 ya Pato la Taifa.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Ofisi ya Taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema utafiti huo umebaini thamani ya Shughuli zisizo rasmi Ni kiasi Cha Shilingi bilioni 6 ambapo Wanawake ndio wameonekana kuwa wengi kwenye Shughuli hizo huku Wilaya za ilala na Temeke zikionekana kuingoza kwa kuwa na Shughuli zisizo rasmi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages