Roman Reigns Akutwa na Corona - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Monday, January 3, 2022

Roman Reigns Akutwa na Corona


Bingwa wa Mkanda wa World Wrestling Entertainment (WWE) Universal Championship, Roman Reigns amekutwa na maambukizi ya UVIKO-19 hivyo kuondolewa kwenye game ya WWE Day One PPV iliyofanyika usiku wa jana State Farm Arena huko Atlanta, Georgia.

WWE.com ilithibitisha ripoti ya awali na kwamba itifaki za kampuni kuhusu COVID-19 hazikumruhusu Reigns kuonekana kwenye ulingo baada ya kupimwa na kukutwa anamaambukizi.

Mabadiliko ya dakika za mwisho kwenye game hiyo yalimfanya Brock Lesnar kuongezwa kwenye mchuano wa WWE kuwania taji la Bingwa wa WWE lililokuwa linashikiliwa na Big E.

Katika game ya watu watano badala ya wanne iliyochezwa ikihusisha Bingwa wa WWE Big E dhidi ya Seth Rollins, Kevin Owens, Bobby Lashley, na Lesnar. Mnyama huyo, the beast aliibuka mshindi nakutwaa taji hilo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages