WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA WASHAURIWA KUPINGA SHERIA KANDAMIZI ZINAZOMINYA UPATIKANAJI WA HABARI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, February 22, 2022

WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA WASHAURIWA KUPINGA SHERIA KANDAMIZI ZINAZOMINYA UPATIKANAJI WA HABARI


Na Farida Said | VYOMBO vya habari na wanahabari kwa ujumla wameshauriwa kuwa mstari wa mbele katika kupinga sheria kandamizi zinazominya uhuru wa habari na upatikanaji wa habari hapa nchini Ili kutoa uwanda mpana katika uandikaji, uchapishaji na utangazi wa habari kwa lengo la kutoa fursa kwa wananchi kupata taarifa sahihi na kwa wakati.

Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Mradi wa Boresha Habari Wakili Msomi Godliver Shayo kwenye mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uandikaji wa habari pamoja na makala katika uwanda wa kilai.

Wakili Godliver amesema kutokana na matukio ya hivi jaribuni ya kufungwa na kufunguliwa kwa vyombo vya habari na kukamatwa kwa baadhi ya waandishi ni moja ya sababu Kituo Cha Sheria na haki za Binaadamu kupitia Mradi wa Boresha Habari kimeona haja ya kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini.

"Kuna tukio la kufunguliwa kwa magazeti ambapo Waziri Nape aliyafungulia magazeti yakiwemo ya Mwanahalisi,Tanzania Daima na Mseto lakini ni vyombo vichache sana ndio vimeripoti kufunguliwa kwa magazeti yale tena na vyenyewe vimeandika kwa juu juu tu, ndio maana tumeona kuna haja ya kutoa mafunzo haya," amesema Wakili Godliver.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania(TEF) Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari nchini kuhakikisha wanafuata Sheria, kanuni na misingi ya uandishi wa habari sambamba na kuwa makini wakati wa utekelezaji wa majukumu hayo.

Kwa upende wao waandishi waliopatiwa mafunzo hayo wamekishukuru kituo Cha msaada wa Sheria na haki za Binaadamu (LHRC) kwa kutoa mafunzo hayo kwani yatawasaidia katika kuandaa mkala za uanda wa kilai zenye ubora na kufuta Sheria pamoja na sera ya habari ya Tanzania.

Mfunzo hayo ya siku mbili yamewakutanisha waandishi kutoka mikoa tofauti nchini ikiwemo Morogoro, Njombe, Mbeya, Dodoma, Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Kiwla, Katavi, Mara, na Arusha ambapo kwa pamoja wamepatiwa mafunzo kuhusu uandishi bora wa makala katika uanda wa kilai pamoja na habari za uchunguzi.

Pia waandishi hao wamepatia elimu kuhusu Sera ya habari nchini sambamba na kanuni pamoja na Sheria ya habari nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages