Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Afrika Mashariki (EACCIA), Charles Kahuthu wakati ujumbe wa viongozi wa chemba hiyo kutoka nchi sita ulipomtembelea ofisini kwake. Ujumbe huo uliambatana na Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR (kushoto). Ujumbe huo umepongeza mkakati wa Benki ya CRDB wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambao unachochea utekelezaji wa mkataba wa Makubaliano ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AFTA). Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Biashara na Viwanda Afrika Mashariki (EATIW) 2022.
Ukuaji wa huduma za kifedha katika Ukanda wa Afrika Mashariki umetajwa kuwa utasaidia kuchochea ukuzaji wabiashara na uchumi wa mataifa wanachama.
Kauli hiyo imetolewa na wataalamu wa masuala ya uchumi nabiashara barani Afrika, baada ya kuzungumza na uongozi wa Benki ya CRDB. Benki hiyo katika miaka ya karibuni imeendelea kutanua huduma zake nje ya Tanzania.
Rais wa Chemba ya Biashara Afrika (AfBC). Dk Amany Asfour akiwa na ujumbe wake uliojumuisha viongozi kutoka chemba zaBurundi,Uganda, Zambia, Botswana, Rwanda, Ethiopia na Misri walikuwa nchini kwa ziara maalumu.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CRDB Jijini Dar es Salaam jana, Dk Asfour aliipongeza benki hiyo kwajitihada za kufungua milango na kuimarisha biashara kwenye nchi hizo.
Alisema mkakati wa CRDB kuziunganisha kibiashara nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, unaendana na jitihada za viongozi wa mataifa hayo ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
“Hatua ya CRDB kutoa huduma nchini DRC ni kuonyesha kwavitendo jitihada za kuimarisha biashara baina ya nchi za ukanda huu na kuhakikisha zinashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mkataba wa makubaliano ya eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AFTA)," alisema Dk Asfour.

Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wajumbe wa viongozi wa Chemba za Biashara tofauti sita (Misri, Zambia, Botswana, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Uganda) walipotembelea makao makuu ya Benki ya CRDB. Wengine pichani ni, Mkurugenzi Mkuu wa EACCIA, Charles Kahuthu, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Congo, Jessica Nyachiro. Ujumbe huo umepongeza mkakati wa Benki ya CRDB wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambao unachochea utekelezaji wa mkataba wa Makubaliano ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AFTA). Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Biashara na Viwanda Afrika Mashariki (EATIW) 2022
Rais wa Chemba ya Biashara nchini Burundi (CFCIB), Denis Nshimirimana alisema kwa kipindi cha miaka 10 ya benki hiyo nchini mwake, mapinduzi makubwa kwenye sekta ya benki yamesaidia kuchochea ukuaji wa biashara.
"Nimefurahi kusikia CRDB inafungua kampuni yake tanzu nchini DRC itakayokuwa na makao yake makuu mjini Lubumbashi. Hatua hii pia itachangia kukuza biashara baina ya Burundi, DRC, Tanzania," alisema Nshirimimana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliushukuru ujumbe huo kwa kutembelea nchini na kuwahakikishia kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo wa nchi zote za ukanda wa Afrika Mashariki.
Nsekela alisema lengo la benki hiyo ni kukuza biashara baina ya mataifa ya Afrika Mashariki, huku akibainisha kuwa kuingia kwa nchi ya DRC katika jumuiya hiyo, kutasaidia kuufanya ukanda huu kuwa imara na shindani kibiashara.
Alisema benki hiyo itaendelea kutanua huduma zake kutokana na sera madhubuti za Serikali zinazohimiza kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi kwa nchi majirani.
"Dhamira ya Rais wetu (Samia Suluhu Hassan) ni kuendelea kufungua milango na kukuza uhusiano wa kibiashara baina yanchi zetu za ukanda huu pamoja na majirani wengine, sisi kama benki tumejipanga kuhakikisha tunashiriki kikamilifu, ikiwamo katika kufanikisha miradi ya pamoja," alisema
No comments:
Post a Comment