
Uwepo wa Makongamano na hafla mbali mbali ya Kidini kutaweza kurudisha Mila Silka na Tamaduni Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo akifungua Tamasha la Ramadhani lililotayarishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofanyika katika kiwanja cha Misuka Mahonda.
Amesema Zanzibar inasifika kwa maadili mema kihistoria yaliyotokana na Dini ya Kiislamu maadili ambayo kwa sasa yamepotea hatua inayopelekea kukosa viongozi bora wenye hapo baadae.

Amesema malezi mema kwa watoto yatasaidia kupata Wanazuoni na Maimamu wa baadae ambao watakuja kuisimamia Dini ya Allah (S.W) ambao pia watasaidia kupata Zanzibar yenye viongozi bora wenye maadili mema.
Aidha Alhajj Hemed amesema kuwa ana Imani Kongamano hilo litakuwa na mnasaba wa Maendeleo ya Zanzibar yenye maadili mema kupitia mada mbali mbali na ujumbe utakaotolewa kwa wawasilishaji mbali mbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Muhamed Mahmoud ameeleza kuwa lengo la kuandaa Tamasha hilo ni kubadili fikra za wananchi wa Mkoa wa Kaskazini na Zanzibar Unguja kwa ujumla ili Zanzibar irudi katika maadili iliyokuwa ikisifika.

Nae Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi amesema ili kurudi katika malezi bora ni wajibu kufuata maelezo yaliyomo katika Qur-an Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W) na kushauri kuundwa kwa Kamati za Maadili katika Shehia.
.jpeg)
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
18 Aprili 2022
No comments:
Post a Comment