"BINADAMU TUNATOFAUTIANA TUHESHIMIANE" MHE.HEMED - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, May 13, 2022

"BINADAMU TUNATOFAUTIANA TUHESHIMIANE" MHE.HEMED

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akitoa salama za Ijumaa Karimu kwa Waumini wa Masjid JAMAEE ALSALAM uliopo Fuoni Wilaya ya Magharibi ‘B’ Zanzibar.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wametakiwa kuendeleza kuiombea nchi yetu ili iweze kunusurika na majanga mbali mbali yanayoweza kujitokeza.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo wakati akisalimiana na Waumini wa Masjid JAMAEE ALSALAM uliopo Fuoni Wilaya ya Magharibi ‘B’mara baada ya kumalizika Swala ya Ijumaa.

Amesema ni vyema kuendeleza kuiombea Zanzibar na kuendeleza Ibada kama ilivyokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuwataka Waislamu na Wazanzibari kwa ujumla kuendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum ili kukuza upendo na kuimarisha amani iliyopo ili Kuisaidia Serikali kwenye masuala ya Maendeleo.
Mhe. Hemed ameendelea kuwataka waumini kushikamana na kuendelea kutoa mchango wa aina tofauti na kuendelea kuitunza Amani iliyopo ili kutoa fursa kwa Wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta mbali mbali na kupelekea kupata Zanzibar yenye maendeleo.

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza Wananchi kuendelea kuwaombea Dua Viongozi Wakuu wa Nchi kuiongoza vyema Zanzibar kwa Busara na Uadilifu ili waweze kuwatumikia wananchi wake.

Akigusia suala la Maadili ndani ya Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anatumia nafasi aliyokuwa nayo katika kuijenga Zanzibar yenye maadili mema na utulivu kwa wananchi wake.
Kwa upande Sheikh SAID HAMID KHALFAN katika Khutba ya Sala ya Ijumaa amewataka waumini kuheshimu Ndoa zao kwa kuacha kutumia neno Talaka kama masihara ili kupunguza migogoro ndani ya Familia.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages