KIJANA AKAMATWA AKITAPELI KWA KUJIFANYA MKUU WA MKOA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, June 17, 2022

KIJANA AKAMATWA AKITAPELI KWA KUJIFANYA MKUU WA MKOA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Warren Max Mwinuka (20) Mkazi wa Makondeko Mbeya Mjini kwa tuhuma za kujifanya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la “juma_homera”.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 07.06.2022 majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John Jijini Mbeya. Mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwaadaa watu kwa kujifanya ni Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu yak wake ili wananchi waweze kutoa/kupeleka kero/shida mbalimbali kwake. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages