MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI YA ANWANI ZA MAKAZI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, June 18, 2022

MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI YA ANWANI ZA MAKAZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa operesheni anwani za makazi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa operesheni ya anwani za makazi kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Juni 18,2022
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa operesheni anwani za makazi, Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Juni 18, 2022 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameagiza Wizara zinazohusika na Zoezi la Anwani na Makazi kutatua Changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika Zoezi hilo.

Mhe. Majaliwa ambae ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya watu na Makazi ameyasema hayo katika kikao cha Tano Cha Kamati hiyo pamoja na Tukio la kukabidhi Taarifa ya utekelezaji wa Operesheni ya Anwani ya makazi iliyofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre Jijini Dar-es-Salaam.

Amesema katika Zoezi la Anwani za Makazi kumejitokeza Changamoto mbali mbali kwa baadhi ya maeneo ambazo zimesababisha kutofanyika ipasavyo kwa zoezi hilo, akitolea mfano wananchi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi kukaa kisheria. Hivyo ni vyema Wizara husika kutatua changamoto hizo na nyenginezo.

Mhe. Majaliwa ametumia Fursa hiyo kuwataka wananchi kuepuka kukaa maeneo yasiyo rasmi kuishi kisheria ili kuepuka athari mbali mbali zinazoweza kujitokeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya watu na Makazi 2022 Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameeleza kuwa Kukamilika kwa Zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi kumetokana na Mashirikiano yaliyopo baina ya Wizara za pande zote mbili za Muungano na kueleza kuwa Mashirikiano hayo yanaongeza Imani kwa viongozi wakuu wa Serikali.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Hemed amewataka Wananchi kuendelea kutoa mashirikiano pamoja na kulinda miundombinu iliyowekwa kwa maslahi ya Taifa.

Nae Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape M. Nawiye ameeleza kuwa Wizara imejipanga kuanzisha Sheria mahususi ya Anwani za Makazi ambayo itasaidia kurahisisha huduma hizo kwa wananchi sambamba na kushirikiana na Wizara ya Elimu katika Kuanzisha mtaalam kwa Skuli.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages