MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA AFANYA UKAGUZI UJENZI WA SOKO MWANAKWEREKWE - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, June 16, 2022

MHE. HEMED SULEIMAN ABDULLA AFANYA UKAGUZI UJENZI WA SOKO MWANAKWEREKWE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa muda wa wiki mbili kuitaka Wizara ya Nchini Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ kukaa na Muwekezaji aliekabidhiwa Ujenzi wa Soko la Jumbi na Mwanakwerekwe na kufuata taratibu za kisheria ili kuendelea na ujenzi wa masoko hayo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa Miradi ya Masoko katika Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ameeleza kuwa hatua iliyofikia katika masoko hayo sio ya kuridhisha jambo ambalo haliendani na Azma ya Serikali ya Awamu ya Nane kwa kushirikiana na Wawekezaji wa ndani na wa nje katika kujenga miradi mbali mbali ya maendeleo.
Aidha Mhe. Hemed amesema kuwa SMZ itaangalia namna bora ya kujenga soko la Jumbi ili kuwasaidia wananchi na wajasiriamali kuweza kupata eneo zuri na la kisasa ambalo wataweza kujipatia huduma zao za kila siku.

Nae waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Muhamed ameeleza kuwa Wizara hairidhishwi kuona wawekezaji kuenda kinyume na makubaliano waliyofunga katika Mkataba jambo ambalo linapelekea kuchelewa ujenzi wa Miradi hiyo.

Katika Ziara hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametembelea ujenzi wa Darajani Bazaar (Soko la Darajani) na kueleza kuridhishwa kwake kwa hatua iliyofikia ambapo ameeleza kuwa kukamilika kwa soko hilo kutasaidia kukuza uchumi wa Nchi na kuwasaidia wananchi kujipatia kipato.
Katika ziara hiyo Mhe. Hemed ametembelea Bandari ya Malindi na kujionea hali ya ushushaji na upakiaji wa Makontena na kuutaka Uongozi wa Shirika la Bandari la Zanzibar kuhakikisha wanaweka mazingira ya kupunguza mrundikano wa Makontena kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa kuyapeleka Makontena eneo la Bwanani ili kurahisisha ushushaji wa Makontena kwa wakati eneo la Bandari.

Aidha Mhe. Hemed amefurahishwa kuona maamuzi ya Shirika la Bandari kuweka One Stop Centre ya Shughuli za Bandari na kuwataka kuharakisha kukamilika kwa Mfumo wa kuendesha Kituo hicho na kueleza kukamilika kwa mfumo huo kutasaidia ukusanyaji wa mapato na kukuza uchumi wa Nchi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages