.jpeg)
Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji ili kuja kuwekeza kwa kukuza pato la nchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo Ofisini kwake Vuga alipokutana na wawekezaji kutoka nchi mbali mbali.
Mhe. Hemed ametumia fursa hiyo kuwakaribisha kuja kuwekeza katika sekta mbali mbali hasa sekta mama ya uchumi wa Buluu.
Aidha Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kuongeza idadi ya watalii nchini kupitia vivutio mbali mbali vilivyopo akigusia baadhi vilivyomo katika filamu ya Royal Tour.
Nae waziri wa Utalii na Mambo ya kale mhe Simai Moh'd Said amesema kuwa Zanzibar ina sehemu nyingi za uwekezaji hasa katika utalii kulingana na mazingira yake yaliyopo Nchini.

Amesema faida kubwa ya Zanzibar ni kuona kuwa wawekezaji wanaongezeka kwa wingi kuja kuwekeza na kueleza kuwa Wizara inaweka mazingira mazuri akitolea mfano kilimo cha Spice na kuboresha miundombimu hasa katika sekta ya Utalii.
.jpeg)

.jpeg)
No comments:
Post a Comment