RC – AMOS MAKALLA AIPONGEZA COSTECH KWA KUENDELEA KULEA BUNIFU NA TAFITI ZENYE TIJA NCHINI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, July 2, 2022

RC – AMOS MAKALLA AIPONGEZA COSTECH KWA KUENDELEA KULEA BUNIFU NA TAFITI ZENYE TIJA NCHINI


Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Amos Makalla awapongeza COSTECH kwa kuendelea kuratibu tafiti na bunifu zenye tija na kutoa suluhisho la wananchi Tanzania kupitia Maonyesho ya 46 ya sabasaba kwa mwaka 2022.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) tarehe 1 Julai 2022 katika Maonesho hayo ya sabasaba.

"Tafiti zinazofanyika zinainisha gaps lilipo ambalo lina maswali yaliyokosa majibu, kwahiyo COSTECH mmekuwa majibu kwa maana watu wanakuja na solutions mbalimbali” alisema Mhe. Makalla

Mhe. Amos Makalla amesema Sera nzuri na mwelekeo Bora alioonyesha Rais Samia Suluhu Hassan kuitangaza Nchi kimataifa hususani Royal tour vimechagiza Maonyesho ya 46 ya sabasaba kuwa na mwamko mkubwa na ushiriki wa Makampuni mengi kutoka ndani na nje ya Nchi.

Aidha, Mhe. Makalla ameongeza kuwa “Nitoe rai kwa wananchi na wanafunzi una idea yako inayoonesha ubunifu popote pale COSTECH watakulea” alihitimisha Mhe. Makalla.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages