
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwahutubia wakufunzi wa Sensa wanaoshiriki mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wakufunzi wa Sensa kutoa Taaluma ipasavyo ili kufanikisha zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Tarehe 23 Agosti mwaka huu.
Mhe. Hemed ambae pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati Kuu ya Sensa ya Watu na Makaazi 2022 ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya Wakufunzi wa Sensa ya watu na Makazi ngazi ya Taifa iliyofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Mkoani Iringa.
Amesema kuwa ni dhahiri Elimu waliyoipata wataitumia ipasavyo katika ngazi zinazofuata akitolea mfano Mikoa, Wilaya, Tarafa na Shehia ili kupata takwimu sahihi na zinazokidhi vigezi na kanuni za Umoja wa Mataifa.
Ameeleza kuwa zoezi la Sensa ya watu na makazi ni Zoezi litakalowezesha kupata takwimu muhimu katika kupanga mipango ya Nchi pamoja na kutekeleza matakwa ya Umoja wa Mataifa.
Aidha Mwenyekiti huyo mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ametumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi wakuu wa Nchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa maelekezo yao katika kuhakikisha Operesheni ya anwani za Makazi inakamilika kwa mafanikio.

Kwa upande wake Waziri Afisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. George Simbachawine ameeleza kuwa Sensa ya Mwaka huu itakuwa ni ya mfano na kueleza kuwa Serikali imeiandaa kwa ufanisi mkubwa ili kufikia malengo.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa pamoja na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapiduzi Zanzibar Bw. Salum Kassim Ali Wameeleza kuwa mafunzo hayo yamejumuisha Washiriki Mia Nne na Kumi (410) ambapo Wakufunzi walioendesha ni wabobezi wa Sensa zilizopita.
No comments:
Post a Comment