ZICOO WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA KUPIGA HATUA KIMAENDELEO - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, September 30, 2022

ZICOO WAKUTANA KUPANGA MIKAKATI YA KUPIGA HATUA KIMAENDELEO

Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatib Hassan akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakati wa mkutano wa Maafisa hao uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR
Katibu wa Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (ZICOO) Makame Khamis Moh’d akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Jumuiya hiyo wakati wakijadiliana juu ya hatua waliofikia ya kuainziasha umoja huo, huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (ZICOO) Raya Hamad akimkabidhi cheti maalum cha usajili mlezi wa Jumuiya hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Hassan Katibu Hassan wakati wa mkutano wa Maafisa hao uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Afisa Mahusiano Mamlaka ya viwanja wa ndege Zanzibar Mulhat Yussuf said akichangia mada wakati wa majadiliano katika mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Afisa Habari Wizara ya kilimo Asha Mohammed Abdul -kadir akichangia mada wakati wa majadiliano katika mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Afisa Habari Mkoa wa Kaskazini Unguja Habibu Othman akchangia mada wakati wa mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Afisa Habari Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Omar Hassan akichangia mada wakati wa majadiliano ya mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (ZICOO) Raya Hamad akizungumza na Maafisa hao wakati wa mkutano wakujadili utendaji kazi katika Jumuiya yao Uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR

Na Bahati Habibu, Maelezo

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatibu Hassan ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali kutambua umuhimu na majukumu ya Maafisa Habari na Mawasiliano katika sehemu zao za kazi.

Wito huo ameutoa wakati akizungumza na Maafisa wa Habari na Mawasiliano wa Serikali katika ukumbi wa Sanaa ulipo Raha leo mjini Zanzibar wa kujadili hatua waliyofikia ya uanzishwaji wa Jumuiya ya Maafisa Habari wa Serikali Zanzibar (ZICOO).

Amesema kukamilika kwa usajili wa jumuiya hiyo kutasaidia viongozi wa taasisi kufahamu majukumu ya maafisa hao pamoja na kuzitatua changamoto zinazowakabili.

Changamoto ziko nyingi na tutajitahidi kukabiliana nazo ili kuhakikisha maafisa wa habari wasimamia majukumu yao ya kuielezea jamii kuhusu utendaji kazi wa taasisi zao" Alisema Mkurugenzi huyo.

Nae katibu wa jumuiya hiyo Makame Khamis Mohamed amesema kuanzishwa kwa jumuiya kutasaidia maafisa wa habari kupata sehemu ya kufikisha changamoto zao na kuchukuliwa hatua zinazostahiki.

Aidha amelezea kuwa jumuiya hiyo itakuwa inawapongeza Maafisa habari wanaofanya vizuri pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa hao ili kuhamasisha utendaji kazi.

Nae Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Raya Hamadi wakati akifunga kikao hicho ameishukuru Idara ya Habari Maelezo kwa kuamua kuwaweka pamoja Maafisa wa habari na Mawasiliano wa taasisi za serikali kwa kuanzisha jumuiya hiyo hatua ambayo itapelekea kuimarika kwa sekta ya habari nchini.

Amesema hatua hiyo itapelekea maafisa hao kuzitangaza Taasisi zao ili ziweze kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Nao washiriki wa mkutano huo wameshukuru kwa kuanzishwa jumuiya hiyo hali itakayosaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages