SALAMU ZA MWISHO
Kuta za nchi hii,
Tutajaza jina lako,
Pale tulipoandika historia,
Za Mashujaa Wenzako,
Ulitufunza na kutupa Rukhsa,
Ili tukue kiuchumi.
Haujatupa Rukhsa tukuage Shujaa,
Umeenda mapema bila wosia,
Japo kitabu umetuachia,
Tuzidi kukuenzi na kusoma hekima zako,
Zenye mithili ya vilindi vya bahari.
Nenda Salama Baba,
Wafikishie salamu za Upendo mashujaa Wenzako,
Waambie bado picha zao zinazurura vichwani mwetu,
Na maneno Yao yakitufikirisha usiku na mchana,
Na ile siku ikifika,
Tutaonana tena ahera.
Paul The Poet
29 Feb, 2024

No comments:
Post a Comment