SMZ KUJENGA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA PEMBA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Wednesday, June 12, 2024

SMZ KUJENGA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA PEMBA

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeeleza Mpango wake wa kujenga Uwanja wa ndege wa Kimataifa kisiwani Pemba utakaoruhusu ndege kubwa kutua kisiwani humo moja kwa moja ili kikifunga kiswa hicho kwa Utalii.

Aidha, imetaja azma ya kuzifungua barabara kubwa zenye hadhi ya juu kutoka Wete hadi Chake na kutoka Chake hadi Mkoani mwishoni mwa mwaka huu ili kukikuza kisiwa Cha Pemba kibiashara na uwekezaji.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo Hotel “the mora” alipozindua jina jipya la hoteli hiyo kutoka la zamani la “Emarald” huko Matemwe, Mkoa wa Kasakazini Unguja.

Dk. Mwinyi amesema tayari Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Pemba ili ndege za kimataifa zitue kisiwani humo.

Akizungumzia maboresho makubwa ya uwanja wa Ndege wa Kimaifa wa Abeid Aman Karume Rais Dk. Mwinyi amesema mara baada ya kukamikila kwa hatua kubwa ya jengo namba 3 ambalo kwasasa linafanya vizuri kimataifa, Serikali pia inafanya matengenezo makubwa kwa “Terminal 1 & 2 na ujenzi mpya wa (terminal 4) ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na Utalii nchini.

Pia, Rais Dk. Mwinyi ametaja faida za uwekezaji nchini, nakueleza kuwa umechangia asilimia kubwa ya maendeleo ya nchi kutokana na kodi wanazolipa wawekezaji kwa Serikali ambazo hutumiwa kuboresha huduma za jamii ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara na mawasiliano, ujenzi wa skuli mpya, hospitali, masoko, pamoja na kusambazwa kwa maji safi na Salama.

Rais Dk. Mwinyi pia, alieleza jinsi uwekezaji unavyofungua fursa nyingi kwa wazawa wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi na wafanyabiashara kupata soko la uhakika la bidhaa zao kupitia mahoteli mbalimbali yaliopo nchini.

Alisema, Serikali huwalazimisha wawekezaji wa maeneo yote kuboresha huduma za jamii maeneo yote yaliyopitiwa na uwekezaji ikiwemo kujenga vituo vya afya, ujenzi wa vituo vya watoto yatima pamoja na mahitaji husika ya maeneo hayo.

Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi alimwagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Uwekezaji, Sharif Ali Sharif kuwasimamia wawekezaji wote kununua mahitaji yote yanayozalishwa nchini kabla ya kuagiza nchi ya nchi ili kutanua fursa kwa wajasiriamali wazawa na wafanyabiashara wa ndani.

Akizungumzia uwekezaji wa “Hotel the mora” Rais Dk. Mwinyi amesema imeekeza zaidi ya dola za Kimarekani milioni 600 pamoja na kutoa ajira 600 kwa wazawa na wenyeji nchini.

Akisifia uzuri na haiba ya kisiwa cha Zanzibar, Mkugenzi Mwendeshaji wa kampuni ya “Tui Group, wamiliki wa “Hotel the mora” Sebastian Abel amesema Zanzibar ni kisiwa chenye hadithi nyingi nzuri zenye kumvutia kila mgeni anaetembelea pia ni zawadi na sehemu salama ya uwekezaji na biashara ndio maana wamevutiwa na kuwekeza nchini.

Naye, Waziri Sharif aliwahakikishia ushirikiano wa hali ya juu wawekezaji wote waliopo nchini pia amesema maendeleo makubwa kwenye sekta ya uwekezaji ni juhudi za Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mamlaka ya kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Saleh Saad Mohamed, amesema “Hoteli the mora” yenye hadhi ya nyota tano inamilikiwa na kampuni ya “Tui Group” ambayo tayari imewekeza nchi zaidi ya dola za kimarekani milioni 500 kwenye sekta ya Utalii kupitia hoteli zake za ‘RIU” iliopo Nungwi, “TUI BLUE” ya Mangapwani na “the mora” ya Matemwe.

Alisema, kampuni ya “Tui Group” pia inatarajia kutambulisha jina lake jengine la “Robinson” ambalo tayari ZIPA imelipatia chei cha uwekezaji wa mdadi mkubwa wenye thamani za dola za kimarekani milioni 50, kupitia kampuni ya “Blackstone Limited”

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, Unguja Rashid Hadid amsema mkoa huo una hoteli 316 kati ya hizo 18 zina hadhi ya nyota tano kwa ujumla wake zinachangia asilimia 61 za pato la taifa kutoka kwenye sekta ya Utalii mkoani humo, aidha ameeleza juu ya mkoa wao unavyotumia utalii wa fukwe kukuza sekta hiyo kupitia Sera ya Uchumi wa Buluu.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages