STANBIC YAANDAA FUTARI KUIMARISHA MAHUSIANO NA WADAU - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Thursday, March 12, 2026

STANBIC YAANDAA FUTARI KUIMARISHA MAHUSIANO NA WADAU

Benki ya Stanbic imeandaa futari maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ikiwa ni sehemu ya kushiriki baraka za mwezi mtukufu wa Ramadan pamoja na kuimarisha mahusiano na wadau wake.

Tukio hilo liliwakutanisha viongozi wa dini, viongozi wa benki pamoja na wateja katika mazingira ya mshikamano na tafakari ya maadili ya kijamii yanayohimizwa katika kipindi hiki cha Ramadhani.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir bin Ally, huku ujumbe wa Stanbic Bank ukiongozwa na Omari Mtiga, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum wa benki hiyo.

Kupitia futari hiyo, Stanbic Bank ilisisitiza dhamira yake ya kuendelea kujenga mahusiano ya karibu na wadau wake huku ikiendeleza maadili ya heshima, mshikamano na utoaji kwa jamii. Tukio hilo pia lilitoa fursa kwa washiriki kubadilishana mawazo na kuimarisha ushirikiano unaochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Omari Mtiga, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum kutoka benki ya Stanbic Tanzania (katikati) akimkaribisha Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally wakati wa futari maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja na viongozi wa dini katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana. Kulia ni Salim Abdallah Muhene. Tukio hilo lililenga kuimarisha mahusiano na wadau pamoja na kushiriki baraka za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally, akipokea zawadi kutoka kwa Omari Mtiga, Mkuu wa Wateja Binafsi na Wateja Maalum, Stanbic Bank Tanzania, wakati wa futari maalum iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja na viongozi wa dini katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana. Kulia ni Wilmont Ishengoma, Mkuu wa Tahadhari Stanbic Bank Tanzania. Tukio hilo lililenga kuimarisha mahusiano na wadau pamoja na kushiriki baraka za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages