RAIS WA ZANZIBAR, DK HUSSEIN MWINYI AMETENGUA NA KUTEUA WAKUU WA WILAYA WATANO ZANZIBAR - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Friday, April 10, 2026

RAIS WA ZANZIBAR, DK HUSSEIN MWINYI AMETENGUA NA KUTEUA WAKUU WA WILAYA WATANO ZANZIBAR

Kati ya hizo, tatu zilikuwa zinakaimiwa na mbili waliokuwa wakuu wa wilaya hizo uteuzi kutenguliwa.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Zena Said, Ali Abdalla Said Natepe ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharib B akichukua nafasi ya Amour Juma Mmanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Natepe alikuwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi. Riziki Daniel Yussuf ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A akichukua nafasi ya Rashid Simai Msaraka ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wengine walioteuliwa ni Dk Said Haji Mrisho anakuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja. Kabla ya uteuzi huo alikuwa katibu Tawala wa wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages