RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA SHEIKH ABUUBAKAR AL-ABASSY, ATOA POLE KWA FAMILIA YA WAZIRI NADIR AL-WARDI - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Saturday, May 2, 2026

RAIS DKT. MWINYI ASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA SHEIKH ABUUBAKAR AL-ABASSY, ATOA POLE KWA FAMILIA YA WAZIRI NADIR AL-WARDI



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika dua maalum ya kumuombea marehemu Sheikh Abuubakar bin Said Al-Abassy.

Dua hiyo imesomwa leo, tarehe 02 Mei 2026, katika Ukumbi wa Majid uliopo Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dkt. Mwinyi amemuelezea mwanazuoni huyo kuwa alikuwa mtu mwema, mwenye upendo, na aliyewafundisha watu wengi elimu ya dini.

Wakati huohuo, Rais Dkt. Mwinyi ametoa mkono wa pole kwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mhe. Nadir Abdullatif Al-Wardi, pamoja na familia yake kufuatia kifo cha baba yao mzazi aliyefariki nchini India.

Rais Dkt. Mwinyi alifika nyumbani kwa familia hiyo, Chukwani Buyu, kutoa mkono wa pole na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha msiba mzito.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages