BENKI ABSA TANZANIA YAENDELEA KUJIZATITI KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA - Wor'Out Media

Wor'Out Media is a premier site for selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the world. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.

Breaking

Tuesday, July 21, 2026

BENKI ABSA TANZANIA YAENDELEA KUJIZATITI KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Mtendaji Mkuu wa Kitengo Cha Wateja wa Makampuni (CIB), wa Absa Group kutoka Afrika Kusini, Bw. Zaid Moola (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wa makampuni (CIB), katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji wakuu wa kitengo cha CIB kutoka Absa Group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi.

Katika kuendeleza ushirikiano na kutambua mchango mkubwa wa wateja wake wa Kitengo cha Corporate and Investment Banking (CIB), Benki ya Absa Tanzania leo imeandaa kikao cha kifungua kinywa cha kukutanisha wadau wa biashara jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimetoa fursa kwa viongozi wa benki na wateja kufanya majadiliano ya wazi kuhusu fursa za ukuaji wa biashara, mwenendo wa masoko, pamoja na mustakabali wa sekta ya biashara nchini Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, amesema benki hiyo inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kifedha zinazolenga kukidhi mahitaji ya wateja wake, hususan makampuni na taasisi zinazofanya biashara kubwa.

Aidha, hafla hiyo ilitumika kuwatambulisha viongozi waandamizi kutoka Kitengo cha Corporate and Investment Banking cha Absa Group, wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Bw. Zaid Moola, ambao walipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wateja wakati wa ziara yao ya kikazi nchini Tanzania.

Ziara ya viongozi hao wa Absa Group inaonesha dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kuimarisha mahusiano na wateja wake pamoja na kutoa suluhisho bunifu za kifedha zitakazosaidia biashara kukua na kustawi.

Hatua hiyo pia inaakisi dira ya Absa ya "Kuwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja... Hadithi Moja Baada ya Nyingine."
Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Makampuni (CIB), wa Absa Group Kutoka Afrika Kusini, Bw. Zaid Moola (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Wateja wa Makampuni wa Kanda ya Afrika, Bw. Sola Adegbesan, wakifurahi katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa jijini Dar es Salaam leo kwa wateja wa makampuni, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji hao kutoka absa group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia), akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance, Bw. Muhammad Shah Newaj, katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wa makampuni (CIB), jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushirikiano wa kibiashara baina yao. Kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji wakuu wa CIB kutoka Absa Group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi. Katikati ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Rwegalulira.
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga akizungumza katika hafla waliyowaandaliwa wateja wa makampuni (CIB), jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. kikao hicho pia kiliwakutanisha wateja hao na watendaji wakuu wa kitengo cha CIB kutoka Absa Group, waliopo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za Kigeni wa benki hiyo, Bi. Irene Rwegalulira, wakati wa hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wa makampuni (CIB), jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Absa Tanzania, Bi. Nellyana Mmanyi, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga na Mkuu wa Kitengo cha Shughuli za kibenki wa benki hiy, Bw. Alred Urasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Wateja wa Absa Group, Bw. Clive Potter (kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wa makampuni (CIB), katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam leo, kama sehemu ya kudumisha ushikiriano wa kibiashara baina yao. Katikati ni Mkurugenzi wa Fedha wa Amref Health Africa, Bw. Damas Nugashe na Mkurugenzi Mtendaji wa Savanna Fibre Tanzania, Bw. Thomas Wenanga.
Mtendaji Mkuu wa Wateja wa Makampuni (CIB) wa Absa Group, Bw. Zaid Moola, baadhi ya watendaji wakuu kutoka Absa Group, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, baadhi ya wafanyakazi na wateja wa CIB, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Sharing Buttons

Pages